Thursday, November 25, 2010

kuwa waziri si kuula.

Na Hafidh Kido.

Ndugu Rais Jakaya kikwete wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, ametangaza baraza la mawaziri. lakini kumekuwa na kauliza za kuwasifia baadhi ya watu walio katika baraza hilo kuwa wameula.

kauli hiyo imeonyesha ni namna gani uongozi unachukuliwa kama kitega uchumi badala ya kujitolea kuwasaidia wananchi wanyoge na wenye kuhitaji maendeleo.

waziri ni mtu wa kulinda na kutetea katiba ya nchi, kadhalika atakwenda kutekeleza sera na amri za Rais; sasa anapotokea nyan'gau akasema mtu alieteuliwa kuwa waziri ameula huwa nashindwa kuelewa.

nilitegemea kusikia kauli za pole kwa watu hao kwa maana wanaingia katika dunia ya lawama na kufanya kazi bila kujali kupumzika, sikukuu, urafiki na familia. hata mambo yao waliyokuwa wakiyafanya kwa siri kabla hawajawa viongozi kwa sasa yatakuwa hayana kificho tena.

ule muda wa kutembea mandari, kula chakula cha mchana na familia na kusherehekea tafrija za kifamilia utapunga sasa. kila wakati tegemea wito wa kulitumikia taifa lako. sasa kuula kuko wapi hapo?

mara nyingi kuula huja pale mtu mwenye wadhifa kama wa waziri kuanza kutumia nafasi yake kulipa visasi kwa wabaya wake na kuanza kufuja mali ya umma na kufisidi wanyonge.

hivyo natoa wito kwa wateule wa nafasi yoyote ya kuteuliwa na rais kuwa, huu si wakati wa kuula, bali kazi kwanza.

No comments:

Post a Comment